Azam

USHINDI wa mabao 2-0 ambao Azam imeupata usiku wa tarehe 14 April, Jumapili kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi dhidi ya Namungo umeifanya kupunguza tofauti ya pointi kati yake na Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kubaki tano.

Yanga ambao waliopo nyuma kwa mchezo mmoja, wanaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 5 baada ya kuichapa Singida Fountain Gate jana mabao 3-0 kwenye uwanja CCM Kirumba, Mwanza.

Mabao yote ya Azam FC yamefunga na kiungo mshambuliaji Kipre Junior dakika ya 62 na 84.

Kwa matokeo hayo, Azam imefikisha pointi 50 na imeendelea kusalia katika nafasi ya pili, wameizidi Simba iliyopo nafasi ya tatu pointi nne. Hata hivyo Azam imecheza mechi 22, wakati Simba imecheza michezo 20 hadi sasa.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumanne, kwa mechi mbili, saa 10 jioni Mtibwa Sugar inayoburuza mkia itaialika KMC kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro na saa 1 usiku itakuwa zamu ya Dodoma Jiji kuikaribisha JKT Tanzania huku zote zikitoka kupata sare katika mechi zilizopigwa jana Jumamosi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here