mgunda ratiba ligi kuu

LIGI Kuu Tanzania Bara inazidi kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa pili ambapo timu zinaendelea kupambania pointi tatu.

Ipo wazi kwamba vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga ilisepa na pointi tatu kwenye mchezo wake Mei 5 2024 ubao uliposoma Mashujaa 0-1 Yanga bao likifungwa na Joseph Guede dakika ya 41 sasa inafikisha pointi 65.

Mei 6 2024 Simba inayonolewa na Juma Mgunda itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Azam Complex.

Matajiri wa Dar, Azam FC wapo Morogoro, mji kasoro bahari watakuwa Uwanja  wa Manungu kuwavaa Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Coastal Union itakuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuwakaribisha Tanzania Prisons.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here