Aliyekuwa bondia nguli wa ngumi za kulipwa Mike Tyson atarejea tena ulingoni kupigana dhidi ya Jake Paul ambaye ni mtaalamu wa mtandao hasa wa YouTube Jake Novemba 15, 2024 kwenye Uwanja wa AT&T mjini Arlington, Texas. Tukio hili litakaloonekana duniani kote kwenye mtandao wa Netflix.
Hapo awali, pambano hilo lilipangwa kufanyika Julai 20, lakini likaahirishwa kutokana na Tyson kuwa na kidonda kilichotokea ndani ya ndege.