KITAIFA

YANGA YAIPELEKA CBE KWENYE UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR

Baada ya jana kuwaondoa Vital’O kwa jumla ya magoli 10-0 kwenye mchezo wa hatua ya awali ya mtoano kuwania kucheza hatua ya makundi ya liigi ya Mabingwa Afrika, Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amethibitisha kuwa wameomba mechi yao ya marudiano dhidi ya miamba ya Ethiopia CBE SA ipigwe Zanzibar.

Yanga itaanzia ugenini mechi hiyo ya Raundi ya Kwanza Klabu Bingwa Barani Afrika, baada ya kuisukuma nje ya Michuano hiyo hatua ya awali Vital’O ya Burundi kwa jumla ya Mabao 10-0. Mechi ya kwanza Yanga ikishinda mabao 4-0 na leo ikikamilisha kalamu ya mabao kwa ushindi wa mabao 6-0.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button