Miongoni mwa mambo ambayo yanampasua kichwa Kocha Fadlu Davids ni pamoja na eneo lake la mwisho la ushumbuliaji na hilo limejidhihirisha katika michezo minne waliyocheza ya kirafiki.
Unaweza kuona katika mabao tisa waliyofunga Simba ni bao moja tu lililofungwa na mshambuliaji wa kati kiasili ambaye ni Steven Mukwala, wakati wakiwa Misri kwa maandalizi ya msimu ujao Fadlu alikiri kuwa na kazi ya kufanya juu ya eneo hilo.
Kuwa na wachezaji wa maeneo mengine wenye uwezo wa kufunga ni faida lakini kocha huyo kutoka Afrika Kusini anataka kuona washambuliaji wake wakiwa na wastani mzuri wa kutumia nafasi ambazo wamekuwa wakizitengeneza.
Akimzungumzia Mukwala ambaye alikuwa akicheza soka la kulipwa Ghana, kocha wa zamani wa Yanga na Azam FC, Hans van der Pluijm anaamini mshambuliaji huyo anaweza kuwa suluhisho ndani ya kikosi cha Simba. “Nimemwona akicheza hapa Ghana, ni kati ya washambuliaji wazuri sana, unajua wapo wachezaji ambao wanaweza kuanza kuonyesha makali yao kwa haraka na wengine huhitaji muda, anaweza kuchanganya mbele ya safari, ni mshambuliaji mwenye nguvu, kasi na maarifa,”