KITAIFA
MZIZIMA DABI AZAM FC YAPOTEZA POINTI TATU
MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamepoteza pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda katika mchezo wa mzunguko wa pili uliokuwa na ushindani mkubwa.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Azam FC 0-3 Simba.
Ni Sadio Kanoute alipachika bao la ufunguzi dakika ya 63 kamba ya pili ni Fabrice Ngoma dakika ya 77 na ile ya tatu ni Duchu dakika ya 89.
Azam FC walikuwa na nafasi yakufunga kipindi cha kwanza walikosa penalti kupitia kwa Feisal Salum aliyegongesha mwamba kipindi cha kwanza.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC.