Mshambuliaji Steven Mukwala wa klabu ya Simba ambaye ni ingizo jipya msimu wa 2024/2025, amezungumza juu ya jinsi anavyoumia kuhitaji kuonyesha kile ambacho mashabiki walikitarajia kutoka kwake.
Ikumbukwe katika utambulisho wa Mukwala alitajwa kama “Straika wa Magoli, Akipiga Waah” na hali ikawa tofauti huku mpaka sasa akicheza michezo Kama Ngao ya Jamii na Ligi kuu mchezo mmoja na Tabora United, lakini bado mashabiki hawajaona kile walichotarajia kutoka kwake.
Amesema “Kila mmoja anaweza kuongea kadri anavyoweza kwa sababu huwezi kuzuia hilo. Natambua bado nina deni kubwa la kufanya ndani ya timu hii ili kufikia malengo, hivyo siwezi kusikiliza maneno ya watu kutokana na kutofanya vizuri,” alisema Mukwala.
“Mashabiki siku zote wanapenda mambo mazuri na siwezi kuwaahidi jambo lolote zaidi ya kuomba ushirikiano wao, suala la kutofunga natambua linawaumiza wengi, ila nalichukulia kama changamoto ambayo inanifanya nipambane zaidi ya sasa.”
Steve Mukwala Mchezaji wa Simba SC