MWAMBA Kibu Dennis ndani ya kikosi cha Simba ni chaguo la kwanza kutokana na uwezo wake alionao katika kutimiza majukumu yake.
Kwenye Ligi Kuu Bara amecheza jumla ya mechi 19 katupia bao moja ilikuwa kwenye Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga na katengeneza pasi tatu za mabao.
Nyota huyo pia kwenye mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Liti alisababisha penalti iliyofungwa na Clatous Chama.
Katika Ligi ya Mabingwa Kibu amecheza mechi 9 kafunga bao moja, katengeneza pasi mojahuku akisabaisha penalti moja ilikuwa mchezo dhidi ya ASEC Mimosas bao lilifungwa na Saido Ntibanzokiza.
AFL kacheza mechi 2 kafunga bao moja ilikuwa dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa.
Kibu amebainisha kwamba kucheza ndani ya Simba ni thamani kubwa na anatambua umuhimu wa kuwa kwenye timu hiyo yenye malengo.