Wakati mashabiki wa soka Tanzania leo wakisubiri kumjua bingwa wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam watakaocheza mechi ya Fainali kuanzia saa moja usiku, mchezo huo utatanguliwa na mchezo wa kuwania mshindi wa tatu utakaowakutanisha Simba dhidi ya Coastal Union.
Simba walishindwa kufuzu fainali baada ya kufungwa 1-0 na Yanga huku Coastal wakilizwa mabao 5-2 na Azam.
Mchezo huo wa mshindi wa tatu utachezwa kuanzia majira yya saa 9 alasiri kwenye dimba la Benjamin Mkapa.