ALIYEKUWA Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Barbara Gonzalez na Sued Mkwabi wametajwa mmoja wapo huenda akaja kuchukuwa nafasi ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba.
Hatua hiyo ni baada ya baadhi ya viongozi wa Simba wako katika kikaango huku wakipewa mtihani wa mwisho kujitathimini kulingana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.
Hatua hiyo baada ya kikao kilichofanyika hivi karibuni chini ya Mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji, baadhi ya wajumbe 21 ambao aliwateuwa mwaka jana na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo inayoongozwa na Salim Abdallah ‘Try Again’.
Imeelezwa kuwa baada ya kikao hicho kilichokuwa mahsusi kuangalia changamoto wanazokutana nazo timu yao. ambacho kimewaweka katika wakati mgumu Mwenyekiti na Mtendaji wa timu hiyo kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri katika michezo yote iliyosalia.
“Ni kweli kikao kilikuwa kina mambo mengi, huku baadhi ya viongozi wamepewa mtihani kuhakikisha tunashinda mechi zilizosalia tukianza na Yanga na zote kuhakikisha tunafikia malengo ikiwemo kutwaa ubingwa au kushika nafasi ya pili,” amesema mtoa habari huyo.
Kuhusu maboresho ya kikosi Kocha Benchikha amehakikishiwa kufanyiwa kazi mapendekezo yake ya msimu ujao ikiwemo suala la usajili kwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa hasa safu ya ushambuliaji,” amesema mtoa habari huyo.