kariakoo dabi

BODI ya Ligi Kuu nchini imemtangaza mwamuzi wa kimataifa, Ahmed Arajiga kuwa ndiye atazisimamia sheria 17 za soka katika mchezo wa NBC Premier League kati ya Yanga dhidi ya Simba.

Arajiga atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga, Kassim Mpanga wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo.

Kariakoo Derby itachezwa Jumamosi ya Aprili 20, 2024 saa 11:00 jioni Uwanja wa Mkapa kwa kila timu zote kuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga ambapo pointi tatu zilikwenda Jwangani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here