Kwa kipindi cha hivi karibuni Ligi yetu imekuwa na ubora mkubwa hasa baada ya klabu mbili za Simba na Yanga kuanza kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Jambo hili limewavutia nyota wengi kuja kuitumikia Ligi hii licha ya ubora wa Ligi kuongezeka bado pia maslahi kwa nyota wengi yameongezeka.
Wakala Ronnie Santos ambaye alisimamia dili la Mlinzi wa klabu ya Yanga Gift Freddy amesema kuwa wakati anamtafuta mchezaji huyo huko alipokuwa akicheza alikuwa akilipwa laki sita pekee lakini kwa sasa akiwa na Yanga analipwa zaidi ya million 12.
“Gift Fred akiwa anaitumikia SC Villa alikuwa analipwa 600k kwa Mwezi, nikamfanyia mpango wa kulipwa zaidi ya 12M kila Mwezi ndani ya Young Africans na jambo hilo likafanikiwa.”