Chama

Kiungo mpya wa ‘Wananchi’ Yanga SC, Mwamba wa Lusaka Clatous Chota Chama kawaaga rasmi ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba SC, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Chama kaandika hivi: “Miaka sita iliyopita nilikuja kama mgeni. Mlinipa malengo na changamoto za kuwa bora zaidi. Sina la ziada zaidi ya heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na usaidizi mlionipa kwa miaka yote (sita) hii, hakuna anayeweza kubadilisha historia tuliyoitengeneza pamoja.
Nawatakia kila la kheri na tuendelee kuonana.”

Fundi huyo wa soka kutoka Mitaa ya Lusaka, siku mbili hizi aliwapa joto mashabiki wa Yanga, baada ya kuacha ‘chata’ la Mnyama kwenye ‘bayo’ yake kule insta.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here