Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, klabu ya Simba SC itafunga usajili wake kwa kumsajili mshambuliaji Lionel Ateba (25) kutokea USM Alger ya Algeria.
Mshambuliaji huyo raia wa Cameroon, atajiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili na Simba SC wamelipa $200,000 (Tsh 542,000,000) kukamilisha usajili huo.
Simba SC imerudi sokoni haraka baada ya kuona safu yake ya ushambuliaji imekosa makali mbele ya lango la adui.
Nyota wa Simba SC wanaocheza nafasi ya ushambuliaji ni Freddy Koublan, Steven Mukwala na Valentino Mashaka.