JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba katika mechi tatu ambazo ni dakika 270 ameshuhudia timu hiyo ikiambulia sare moja, ikishinda mechi mbili.
Ni dakika za moto uwanjani kutokana na wachezaji wa kikosi cha kwanza kutokuwa fiti ikiwa ni pamoja na Kibu Dennis aliyepata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Namungo, Henock Inonga ambaye ni beki alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
Mbali na kushuhudia ushindi huo pia kashuhudia wachezaji wa timu ya Tabora United wakimzonga mwamuzi wakiamini kuwa pigo la Najim Musa dakika ya 77 ilikuwa ni bao Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo uliochezwa Mei 16, wachezaji wa Simba walimpa nafasi Musa kupiga shuti kali akiwa nje ya 18 likamfuata Ayoub Lakred ambaye alikuwa langoni.
Pia ni mabao sita Simba imefunga katika mechi zote ilikuwa mwendo wa mbilimbili, Namungo 2-2 Simba, Simba 2-0 Mtibwa Sugar, Simba 2-0 Tabora United.
Kituo kinachofuata ni Mei 9, Azam FC v Simba, Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo wa Mzizima Dabi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.