Beki wa timu ya Taifa Ureno Pepe ametangaza kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 41, baada ya kucheza kwa miaka 23 mfululizo.
Pepe alipata mafanikio makubwa akiwa na Real Madrid, ambapo alipata mataji matatu ya UEFA Champions League na mataji matatu ya La Liga.
Akiwa na Ureno Pepe aliweka heshima kubwa baada ya kucheza mechi 141 huku akitwaa mataji makubwa kama Euro 2016 na UEFA Nations League 2019.
Kufuatia hatua hiyo Cristiano Ronaldo ambaye ni rafiki kwa miaka yote hiyo wa Pepe ameandika ujumbe wa kumtia moyo na kufurahia maisha ya soka pamoja na Pepe.