INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, kuna uwezekano akakosekana kwenye mchezo ujao wa ligi.
Ni nyota Joshua Mutale yeye kwa upande wake mambo bado kutokana na kutokuwa fiti kwa sasa wakati timu hiyo ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Fountain Gate.
Nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ndani ya msimu wa 2024/25 wa Simba uliochezwa Uwanja KMC, Mwenge baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 Tabora United.
Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kuna hatihati nyota huyo akaukosa mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia kubwa mpaka sasa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, kwenye mahojiano na Azam TV ameweka wazi kuwa kwa sasa anaendelea na matibabu ili kurejea kwenye ubora wake.
“Kuna asilimia kubwa ya kukosa mchezo dhidi ya Fountaine Gate kwa mchezaji wetu Joshua Mutale kwa kuwa anaendelea na matibabu alipata maumivu ya nyama za paja atakuwa nje kwa muda wa siku tano.
“Mara baada ya mchezo wetu dhidi ya Tabora United tayari kikosi kimeanza maandalizi kuelekea mchezo wetu huo ambao ni muhimu kwetu kikubwa ni kupata pointi tatu kwani bado timu haijawa kwenye muunganiko mzuri.”
Agosti 25 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa wababe hao kukutana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ndani ya ligi.