Mchezaji ambaye anacheka katika kikosi cha Yanga nchini Tanzania ambaye ni raia ya Ivory Coast hajaonekana katika michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ijapokuwa yupo katika kiwango bora kwenye kikosi chake cha Yanga.

Waziri wa michezo nchini Ivory Coast Mhe. Adjé silas amesema hajui kama mchezaji Pacome Zouzoua anakiwasha kwa kiwango cha kuogopesha kwenye ligi ya Tanzania. Ndio maana hajashangaa kutomuona kwenye kikosi cha timu ya taifa.

Hayo ameyasema leo tarehe 26, January 2024 alipozungumza na Waziri Dr. Damas Ndumbaro alipomuuliza (kwa utani)- Kwanini nyota huyo wa Yanga hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast?

Mazungumzo ambayo yamejadili juu ya kusaini makubaliano maalum ya ushirikiano (MOU) katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo mbili ili kuibua na kukuza vipaji.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here