YANGA hii unaifungaje? Mashabiki wametuma tambo kimtindo kwa watani zao wa jadi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa.
Ngoma imemalizwa dakika 44 za kipindi cha kwanza baada ya Simba kufanya makosa kwenye kuokoa mpira ambao ulionekana hauna madhara kwenye miguu ya Pacome Zouzoa ambaye alimpa pasi Prince Dube aliyemuachia Maxi Nzengeli.
Nzengeli ambaye alikuwa kwenye ubora wake alimtungua kipampya wa Simba Moussa ambaye ameonekana kuwa kwenye ubora wake katika mchezo licha ya kufungwa.
Mwamuzi wa kati Elly Sassi alifanya kazi yake kupeleka mpira kati mara moja ikiwa ni kipindi cha kwanza na mpaka dakika 45 zinagota mwisho ngoma ilikuwa ni Yanga 1-0 Simba.
Fainali ni Agosti 11 2024 Yanga v Azam FC huku Simba ikicheza mchezo wa hatua ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.