KISA PESA ZA WAARABU, ISHU YA INONGA NA SIMBA NGOMA BADO NGUMU
Klabu ya soka ya Simba SC imeanza maandalizi ya kumsainisha nyota wake wa kimataifa wa Congo D, Henock Baka kusalia klabuni kwa msimu mungine zaidi.
Inonga ambaye ni beki kinara wa Simba amebakisha miezi 14 kwa mkataba wake na Simba kutamatika kabla ya kuwa mchezaji huru.
Mapema mwezi uliopita vilabu vya Rabat na Berkane zilionyesha nia ya kuhitaji huduma yake baada ya michuano ya Afcon.
Soko la Inonga linatajwa kuongezeka baada ameonesha kiwango bora kwenye michuano ya AFCON iliyomalizika jana akiisaidia timu yake ya Congo kufika nusu fainali na kumaliza katika nafasi ya nne kwenye michuano hiyo.
Hata hivyo Simba watakumbana na upinzania mkali katika kumshawishi aongeze mkataba mpya haswa ikizingatiwa kuwa klabu za Al Ahly, FAR Rabbat ya Morocco zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kwenye dirisha kubwa la usajili wa wachezaji.