UONGOZI wa Yanga umefunguka na kudai kuwa Mshambuliaji wao, Clement Mzize hawatamuuza na kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa misimu mingine.
Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema hakuna klabu au timu inayoweza kumnunua Mzize kwa sababu bado yupo kwenye mipango ya klabu hiyo.
Amesema Mshambuliaji huyo mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu na wako kwenye mipango ya kumuongeza kwa sababu ni tegemeo kwa nyota wazawa.
“Hatuna mpango wa kumuuza Mzize, kuhusu Kaizer Chiefs tulikuwa naye japa Nabi tena alikuja klabu, ingekuwa mipango hiyo ninaimani jambo hilo lingefanyika kabla halijafika nje ya klabu,” amesema Kamwe.
Amesisitiza kuwa hawana mpango wa kuachana na wachezaji wao muhimu wenye uwezo mkubwa hali iliyopelekea kutoa kiasi kikubwa cha fedha kumbakiza kiungo wao Stephane Aziz Ki.