Mchezaji wa Tanzania, Saimon Msuva ambaye amesajiliwa na timu ya Al Najmah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia amesema safari hii atajitahidi kuhakikisha Saudia inamtambua kwa kuonyesha kiwango bora kwenye timu hiyo kwani tayari ana uzoefu mkubwa na Ligi hiyo kwamaana alishawahi kupita katika Ligi hiyo akiwa na timu ya Al-Qadsiah aliyoichezea kwa msimu mmoja tu

“Malengo yangu ni kucheza kwa muda mrefu kule Saudi Arabia. Sina wasiwasi na hilo kwa sababu naifahamu vyema ile ligi daraja la kwanza na nilishacheza. Nilicheza pale kwa msimu mmoja na bahati mbaya uongozi wa timu ulibadilika hivyo sikuweza kuendelea ingawa nilitamani kucheza kwa muda mrefu zaidi”

“Lakini kwa sasa nina uzoefu wa kule na nimejiandaa kuhakikisha malengo yangu yanatimia. Kikubwa sio ligi nyepesi hivyo jambo la msingi ni kupambana ili kuweza kuisadia timu yangu,” amesema Msuva.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here