WAKIWA kwenye mbio za kujinasua kutoka nafasi ya tatu waliyodumu kwa muda mrefu msimu wa 2023/24 orodha ya wachezaji ambao hawapo fiti imeongezeka.
Aprili 30 kwenye funga Aprili waliambulia sare ugenini huku wakikosa huduma za nyota wao ambao wapo kwenye program maalumu kurejea kwenye ubora wao.
Wakati ubao ukisoma Namungo 2-2 Simba wakigawana pointi mojamoja zinazoifanya Simba upoteza pointi mbili na hata ikishinda mechi zake mbili mkononi bado itabaki hapohapo nafasi ya tatu kiungo mshambuliaji Kibu Dennis alipata maumivu.
Kibu alikwama kukomba dakika 90 kwenye mchezo huo Uwanja wa Majaliwa na mikoba yake ilibebwa na Pa Jobe ambaye hakuwa na siku nzuri kazini.
Mbali na Kibu wengie ambao hawapo fiti ni pamoja na Shomari Kapombe, Clatous Chama, Henock Inonga, Aishi Manula.
Viungo wa kazi ikiwa ni pamoja na mkali wa mapigo huru Saido Ntibanzokiza kiungo wa kazi ngumu Sadio Kanoute hawa wote hawapo fiti.
Meneja wa Idara ya Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema kuwa wakiwa vitani orodha ya wapambanaji wao inazidi kupungua lakini wanaamini watarejea kwenye ubora wao.