MWANASHERIA wa Simba, Hosea Chamba amesema wanasubiri hukumu kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji juu ya wachezaji Awesu Awesu na Valentino Mashaka.
.
Nyota hao waliosajiliwa hivi karibuni mashauri yao yalisikilizwa jana katika ofisi za TFF, kutokana na klabu za Geita Gold na KMC kuishtaki Simba.
.
“Awesu na Mashaka sisi tumewasajili wakiwa wachezaji huru hivyo uwepo wa kesi kutoka timu hizo mbili tunasubiri hatma zake kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji,” amesema Hosea Chamba.