Gamondi

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wana njaa ya kupata alama tatu baada ya kupishana nazo kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kwamba Aprili 24 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Meja Isamuhyo ulisoma JKT Tanzania 0-0 Yanga wote wakagawana pointi mojamoja.

Pointi hiyo inawafanya Yanga kufikisha pointi 59 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 23 leo inakabiliana na Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Azam Complex.

Gamondi amesema: “Tumetoka kucheza mchezo kwenye mazingira magumu na tuna njaa ya kupata alama tatu. Wachezaji wapo tayari hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Hautakuwa mchezo rahisi kwasababu Coastal ni wazuri kwenye kuzuia mashambulizi, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wetu,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here