“Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kutufikisha wote hapa na kwa niaba ya Wanasimba wote naomba kumpongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kwa uongozi wake bora na mchango wake mkubwa wa kuendeleza michezo nchini.”
“Hii ni safari ya pamoja na kwa pamoja tutafanikisha maono makubwa. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Simba Sports Club imepata mabadiliko makubwa ambayo yanalemga kuimarisha klabu yetu.”
“Kujenga upya Simba kumekuwa na gharama kubwa lakini ni hatua muhimu sana. Tumeweza kusajili wachezaji 14 na Mpanzu tumemleta. Hii ni hatua muhimu katika kujenga kikosi imara ambacho kitaweza kushindana katika ngazi ya juu.”
“Tumepata kocha mpya, Fadlu Davids pamoja na benchi mpya la ufundi, kuimarisha miundombinu sahihi ni muhimu katika kufanikisha maono yetu. Tunaendelea kubuni mifumo mipya, bodi imara na kwa pamoja tutahakikisha kila hatua inachukuliwa kwa umuhimu sana.”- @moodewji