USAJILI Uliokamilika Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, usajili Mpya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025, Sajili Mpya za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, Usajili Uliokamilika Azam FC 2024/2025,Usajili Uliokamilika Simba SC 2024/2025,Usajili Uliokamilika Yanga SC 2024/2025, Usajili Mpya Azam FC, Usajili Mpya Simba SC, Usajili Mpya Yanga SC.
Klabu ya Yanga imemuongezea Mkataba wa miaka miwili Mlinda lango nambari moja, Djigui Diarra ambao utamfanya asalie Jangwani hadi mwaka 2026
Klabu ya Yanga imemuongezea mkataba wa miaka miwili, Farid Mussa kuendelea kuitumikia Young Africans SC hadi 2026.
Klabu ya Azam FC imefikia makubaliano na klabu ya El Merreikh ya Sudan ya kumnunua moja kwa moja golikipa, Mohamed Mustafa baada ya mkataba wa awali wa mkopo kumalizika ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomfanya kusalia Azam FC hadi mwaka 2026.
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha saini ya aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 33.
Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Joshua Mutale raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 22 Kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Power Dynamos ya kwao Zambia.
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Steven Mukwala raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 24 kutoka Asante Kotoko ya Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun kutoka Geita Gold FC iliyoshuka Daraja kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza.
Klabu ya Yanga SC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Agee Basiala Amongo mwenye umri wa miaka 25 kutoka klabu ya Maniema ya DR Congo Kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kukamilisha usajili wa Kocha wa Viungo (Fitness Coach), Marouene Slimani kutoka Africain Club ya Tunisia.
Klabu ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza imetangaza kukamilisha usajili wa Kocha, Goran Kuponovic mwenye umri wa miaka 57.
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Kiungo, Yusuph Kagoma kutoka Singida Fountain Gate Kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa winga, Joshua Mutale Mutale mwenye umri wa miaka 22 kutoka Power Dynamos ya kwao Zambia Kwa mkataba wa miaka mitatu.
Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars
umefanya maboresho kwenye Benchi lake la Ufundi kwa kumuongeza Ramadhani Nsanzurwimo kama Kocha Msaidizi na Mchambuzi wa Video (Video Analyst).
Nsanzurwimo ni kocha mwenye leseni ya Diploma A ya CAF ambaye ana uzoefu wa kufundisha timu mbalimbali ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini, Malawi, Mauritius, Burundi na Rwanda.
Kocha wa klabu ya Yanga, Miguel Angel Gamondi amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kukinoa kikosi hicho hadi 2026.
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kukamilisha usajili wa aliyewahi kuwa kocha wa Simba SC, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji kuwa kocha Mkuu wa Klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa FC ya Kigoma. Adam mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.
Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Jhonier Blanco mwenye umri wa miaka 23 raia wa Colombia kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya mji wa Rionegro, inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia Kwa mkataba wa miaka minne.
Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo, Ever Meza mwenye umri wa miaka 23 kutoka klabu ya Leonnes ya Colombia baada ya kumsainisha mkataba wa miaka minne.
Klabu ya Azam imefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) kumsajili kiungo mshambuliaji, Franck Tiesse mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa 2024-25.