KITAIFA
SIMBA BADO INAGAWA DOZI, YASHUSHA KIPIGO CHA 2-1 KWA TIMU YA SAUDIA
Klabu ya Simba imeshinda magoli 2-1 dhidi ya klabu ya Al Adalah ya ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia kwenye mchezo wa tatu wa maandalizi ya msimu (Pre Season) uliochezwa kwenye dimba la Suez Canal nchini Misri.
Kwenye mchezo huo magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji wapya Steven Mukwala dakika ya 9 na Joshua Mutale dakika ya 32.
Huo ni mchezo wa tatu wa Simba baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 dhidi ya Canal SC, jana kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt kwenye michezo hiyo ya ‘Pre Season’.