KITAIFA

FOUNTAIN GATE KAMA MBWAI IWE MBWAI

HAWANA jambo dogo Fountain Gate kutokana na kuweka wazi kwamba wana jambo lao kubwa ndani ya Agosti 2024 ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajia kuanza Agosti 16 2024.

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2023/24 taji la ligi lipo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi pia taji la CRDB Federation Cup lipo mikononi mwa Yanga.

Kuna matamasha yanatarajiwa kufanyika kuelekea msimu wa 2024/25 ikiwa ni Simba Day Agosti 3 2024. Mwananchi Day la Yanga linatarajiwa kuwa Agosti 4 2024 pia kuna Big Day ya Singida Black Stars na Fountain Gate nao wanakuja na jambo lao Agosti 9 2024.

Issa Liponda maarufu kama Issa Mbuzi ambaye ni Ofisa Habari wa Fountain Gate mesema: “Tukutane Agosti 9 2024 Tanzanite Kwaraa Stadium, ishakuwa Mbwai acha iwe mbwai tu mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Siku hiyo itakuwa maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya watakaopeperusha bendera kwenye mechi za ushindani na kutakuwa na mchezo wa kirafiki hivyo sio ya kukosa kila kitu kinakwenda vizuri.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button