KIMATAIFATETESI ZA USAJILI
MBWANA SAMATTA KUUNGANA NA MSUVA, SAUDI ARABIA

Nyota wa kimataifa wa Tanzania ๐น๐ฟ anayecheza soka la kulipwa katika timu ya PAOK ya Ugiriki, Mbwana Samatta โPopatโ inaelezwa anajiandaa kumfuata Simon Msuva anayecheza soka nchini Saudi Arabia ๐ธ๐ฆ baada ya klabu ya Al Kholood iliyopanda Ligi Daraja la Pili nchini humo kutuma maombi ya kumtaka nahodha huyo wa Taifa Stars kwa mkopo.
Kama dili hilo litakamilika huenda Samatta akakutana na pacha anayecheza naye Taifa Stars, Msuva anayeichezea Al Najma katika ligi hiyo. Samatta amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya kikosi cha PAOK na mkataba alionao na Wagiriki hao unatarajiwa kutamatika Juni, mwakani.