Simba

Simba imeanza vibaya mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 na bingwa mtetezi Al Ahly katika wake wa nyumbani wa Uwanja wa Mkapa.

Bao la Ahmed Nabil Koka dakika ya 4 limetosha kuingoza Al Ahly na kutanguliza mguu mmoja nusu fainali ya mashindano hayo.

katika mechi ya mkondo wa pili Simba itahitaji ushindi kuanzia mabao 2 na kuendelea na isiruhusu bao katika mechi ya marudiano itakayopigwa Cairo, Misri, Aprili 5, 2024.

Simba imeingia robo fainali ya michuano hii mara nne katika miaka sita huku mara moja ikitinga Kombe la Shirikisho Afrika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here