Manchester United wanapanga kuweka dau la £50m kumnunua mshambuliaji wa Brightonl, Evan Ferguson huku kukiwa na wasiwasi kwamba Chelsea inaweza kujaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 19. (Daily Star on Sunday)
Wakati huo huo, Mashetani Wekundu wanaweza kumpa mlinzi wa kulia wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka malipo ya pauni milioni 5.6 ili kufidia upungufu wa mshahara wake katika klabu ya West Ham huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akikaribia kuhamia The Hammers. (Manchester Evening News)
Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Giovanni Manna anasema mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Chelsea na Paris St-Germain, ameomba kuondoka kwenye kikosi hicho cha Serie A. (90 min)
Aston Villa bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Ureno Joao Felix lakini uhamisho wowote wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 utafanyika tu ikiwa Atletico Madrid watakuwa na uhalisia kuhusu mahitaji yao ya kifedha. (Mirror)
Villa na Real Betis ni miongoni mwa timu zinazomtaka kiungo wa kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 28, ambaye ataruhusiwa kuondoka Tottenham. (Fabrizio Romano)
Wolves wako tayari kufikiria ofa za €20m (£17.1m) kwa mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 22 Fabio Silva, ambaye anavutiwa na Espanyol, Genoa, Valencia na Wolfsburg. (Team talk )
Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro amehusishwa na kuhamia Saudi Arabia lakini meneja wa Manchester United Erik ten Hag anasema hatarajii mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford msimu huu wa joto. (Metro)
Crystal Palace wako kwenye mazungumzo na Wolfsburg kuhusu kumsajili beki Mfaransa mwenye umri wa miaka 24 Maxence Lacroix kutoka klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sports Ujerumani)
Palace na Aston Villa wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea Trevoh Chalobah baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuzuiwa kwenye kikosi cha kwanza cha The Blues (Telegraph )
Bournemouth wanakaribia kumsajili mlinzi wa Mexico Julian Araujo, 22, kutoka Barcelona kwa mkataba wa thamani ya €10m (£8.6m). (ESPN)