Mwandishi Nguli wa Michezo nchini Dominick Salamba amefunguka sakata la kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki bado kusaini nyongeza ya mkataba mpya, ametoa ufafanuzi huu hapa chini;-
ALICHOKISEMA HIKI HAPA>>ย Aisee hakuna siku nimepokea simu nyingi za maswali kama hii leo,
Wengi wakihitaji ๐ฝ๐๐๐ฃ๐๐ซ๐๐ ๐จ๐ ๐ธ๐๐ฃ๐๐๐ nitolee ufafanuzi kuhusu sakata la Azizi Ki na Yanga SC,
โข Je,mkataba umesainiwa au bado?
โข Je,Azizi Ki amepokea Offa kutoka timu zipi?
KWANZA NIANZIE KWENYE CHANZO:
Kuna muandishi mkubwa kutoka Ghana,leo hii ametoa chapisho kuwa Azizi Ki hajasaini mkataba wowote ule na Yanga SC mpaka sasa,
Binafsi naheshimu sana wanahabari na vyanzo tofautitofauti vya taarifa,lakini em, tujikumbushe kidogo:
โข Huyo mwandishi ndiye aliyetuaminisha kuwa Azizi Ki amesaini Simba SC kutokea Asec Mimosas na tena akatutajia hadi gharama zilizotumika na mshahara atakaopokea,
โข Mwandishi huyo huyo aliwahi kutuaminisha kuwa Adebayor amesaini Simba SC na ataichezea timu hiyo,
โข Aliwahi kutuaminisha kuwa Cesar Manzoki amesajiliwa Simba SC na akangโangโania kwelikweli ila kilichofuata sote ni mashahidi.
MAANA YANGU NI NINI:
Huyo mwandishi wenu hajaanza leo kuupumbaza Umma kwa taarifa zake FAKE kuhusu sajili na isitoshe alishajipambanua yeye yuko upande gani wa ushabiki kwa timu za Bongo,
Hajaanza leo kutoa taarifa asizozijua (iwe kwa kujua au kutokujua)
MUSTAKABALI WA AZIZI KI:
Hapa sitajielezea sana ila nawakumbusha tu:
โขย Wakala wa Azizi Ki alikuja Bongo na akaenda hadi Zanzibar kutazama fainali ya kombe la CRDB ambalo Yanga SC alilitwaa,
โขย Baada ya pale hamkusikia tena mijadala kuhusu Azizi Ki huku mitandaoni,kwanini?
โขย Je huyo wakala wake alikuja kucheza?
โขย Swala la Azizi Ki kusaini mkataba mpya lilishamalizika kitambo na hata hivi sasa Azizi Ki ameshaanza kula mshahara wa mkataba mpya.
BONUS:
โขย Rejea kauli ya Azizi Ki akiongea na Privadinho kupitia InstaLive,
โขย Azizi Ki aliahidi kuwa atapambana kuzalisha assists nyingi ili kumsaidia Prince Dube awe Top Scorer msimu unaofuata (Swipe kuona video)
โขย Azizi Ki hakuishia kusaini mkataba mpya tu,alishaweka na malengo yake ya msimu unaofuata akiwa na Yanga SC.
NB:
๐ฝ๐๐๐ฃ๐๐ซ๐๐ ๐จ๐ ๐ธ๐๐ฃ๐๐๐ nikishazungumza,hakuna wa kuongeza neno,maana huwa namaliza kila kitu.
NBยฒ:
OUTSIDE THE PITCH,FOOTBALL IS ALL ABOUT BUSINESS รฑ MIND GAMES.