Chadrack Boka kusajiliwa yanga

Miguel Gamondi ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 na hata msimu uliopita michezo mingi uliwaona Yanga SC wakiutumia zaidi mfumo huo ambao unatumiwa zaidi na timu zinazofanya pressing kama ilivyo kwa Yanga SC.

Ingizo jipya la mlinzi wa kushoto Chadrack Boka linaebda kuufanya mfumo huo kukamilika zaidi kutokana na uwezo wake wa kuoverlap kwenye lango la mpinzani.

Ukiangalia vyema formation ya 4-2-3-1 haswa kwa upande wa Yanga SC unaona wale watatu wanaoenda kucheza nyuma mshambuliaji kwa asilimia kubwa ni viungo washambuliaji na sio mawinga asilia hivyo watakuwa invited winger watacheza zaidi ndani.

Hapo ndipo utakapo waona Chadrack Boka na Kouasi Yao wakiutanua uwanja na kwenda kucheza kwenye mstari huku wakiingia kwenye box kupiga V pass au krosi ndani ya kwenye sita.

Watu watajiuliza kuhusu nafasi za Boka na Yao wakipanda na timu ikaporwa mpira na wapinzani wakafanya Counter Attack jibu ni jepesi sana yupo Destroyer Khalid Aucho ‘The Tank’.

Khalid Aucho atarudi nyuma na katikati ya walinzi watatu ambao watakuwa wamesalia nyuma na kutengeneza back 3 ya yeye Job na Bacca hawa wata sio rahisi kupitika wapo imara mnoo kwenye mbinu za kuzuia huku langoni pia kuna Swiper Goalkeeper, Djigui Diarra ambae anaweza kunusa hatari ya long ball na kuikoa timu.

Kimsingi Chadrack Boka anaenda kukamilisha mfumo wa 4-2-3-1 wa mwalimu Miguel Gamondi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here