MIKONO ya kipa namba moja w Coastal Union, Ley Matampi ilikuwa ni moto wa kuotea mbali kutokana na kuokoa hatari za wapinzani wao Yanga.


Licha ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Yanga 1-0 Coastal Union, kipa Matampi alifanya kazi kubwa kwenye kutimiza majukumu yake.


Miongoni mwa nyota ambao walifanya majaribio makubwa kwenye kumtungua kipa huyo ni pamoja na Aziz KI ambaye mapigo yake yalikuwa yanagotea kwenye mikono ya kipa huyo.


Guede ambaye alifunga bao moja dakika ya 76 naye pia pigo lake moja liligonga besela na kuokolewa na mwamba huyo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Yanga ni namba moja kwenye ligi wakiwa na poointi 62 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here