Baada Simba ya kutolewa kwenye Klabu bingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali, pamoja na CRDB Bank Federation Cup kumekuwa na maneno mengi ambapo Afisa habari wa Simba Ahmed ally kupitia ukurasa wake ameandika.

“Timu yetu inapitia kipindi kigumu Lakini ni tofauti na inavyozungumzwa yaani wanaongeza chumvi

Huu ni mpango wa makusudi unaoratibiwa na wasiotutakia mema, Bahati mbaya ni kwamba Wana Simba tumeingia kwenye mtego wa kujidharau na kujitukana

Tukiwa na Simba Bora sana tuliwahi kutolewa hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na UD Songo, Tukiwa na Simba Bora  tuliwahi kutolewa na Green Warrios kwenye Kombe la Shirikisho

Haya mi Maisha ya kawaida kwenye mpira wa miguu

Kila timu ya mpira hupitia nyakati kama hizi, Ila tukipitia Simba basi huonekana ni kitu cha ajabu inawezekana tunahukumiwa na ukubwa wetu

Leo watakuambia wachezaji wabovu, kesho Muwekezaji tatizo, kesho kutwa Viongozi hawafai

Hivi tungekua na matatizo yote hayo si tungekua tumeshuka daraja?

Wengine wanaibuka kukashifu viongozi na kudhihaki wachezaji wakiamini huko ndio kuipenda Simba au wao ndio wenye uchungu sana na Simba

Wakati Nyuma Mwiko wako dhofli hali waliibuka na kauli ya kusema tumeipenda wenyewe acha ituue, Hii ilikua kauli ya kishujaa sana na waliamua kufa na timu yao

Kwa sasa hatuna budi kusimama na timu yetu ili mambo yasiharibike zaidi, hatuwezi kubadili yaliyopita ila tunaweza kutengeneza yajayo

Tulichobakiwa nacho ni Ligi Kuu ya NBC, Kwa pamoja tuwekeze nguvu kwenye kombe hili

Tuache kulaumiana, tuhamishie machungu yetu na tuelekeze hasira zetu kwenye ligi

Pengo ni alama 4 tukisimama sawa sawa kwa umoja wetu tunaliondoa

Hii inaanza na mechi ya Tarehe 13 dhidi ya Ihefu, na baada ya hapo mechi ya tarehe 20, tukichukua alama 6 kwenye mechi hizi tutakua pazuri sana”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here