Zikiwa zimesalia siku mbili kuelekea ‘dabi ya kariakoo’ ya Simba na Yanga itakayochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua amesema anataka mashabiki wa Yanga wafurahie kipaji chake na kwa kuanzia anataka kuanza na mchezo wa Agosti 8.
Staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amesema licha ya ushindani wa namba ndani ya timu yao kuwa mkubwa, lakini anataka kuwa na kitu tofauti ili kuhakikisha kwamba anapata nafasi na kufanya makubwa.
“Mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wetu kusajili wachezaji wazuri wenye ubora. Lakini sisi kama wachezaji tunatambua umuhimu wa matokeo mazuri kwenye mchezo mkubwa kama huo.”