MWAMBA HUYU ATAMBULISHWA SIMBA
KIUNGO mkabaji Augustine Okejapha ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kupata changamoto mpya kwa msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti.
Nyota huyo ni raia wa Nigeria anatarajiwa kuwa kwenye changamoto mpya kwa msimu wa 2024/25 ndani ya Simba.
Julai 5 2024 Simba ilimtambulisha kocha mpya ambaye ni Fadlu Davis ambaye atafanya kazi na ingizo hilo jipya pia.
Ana miaka 23 nyota mpya wa Simba akitajwa kuwa kwenye kazi kubwa katika eneo hilo la ukabaji ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ukiweka kando nyota huyo pia Simba ilimtabulisha Valentino Mashaka ambaye ni kiungo mshambuliaji alikuwa akikipiga Geita Gold na mchezaji wa kwanza kutambulishwa alikuwa ni beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union.