Malu Stonch amefariki dunia

Mwimbaji wa Muziki wa dansi wa kundi la FM Academia, Malu Stonch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, taarifa zinasema kuwa Malu alifariki baada ya kuanguka ghafla jukwaani akiwa anatekeleza majukumu yake ya kuimba na bendi yake ya FM Academia katika ukumbi wa Target, Mbezi Beach.

Mwanamuziki huyo wakati anaimba alidondoka ghafla na kuangukia uso na kupoteza fahamu huku damu zikimtoka masikioni na kung’ata ulimi ndipo wakampa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka Hospitali ya Masana, Mbezi beach na baada ya kufika Hospitalini hapo madaktari walisema kuwa tayari alikuwa ameshafariki dunia.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here