SIMBA YAKWAMA PIA KUONDOKA NA USHINDI MBELE YA IHEFU

mambo bado yamekuwa magumu kwa Simba ambapo leo wameondoka na sare ya dhidi ya Ihefu waliokuwa nyumbani kwenye mchezo wa ligi kuu bara.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti umesoma Ihefu 1-1 Simba ambapo waligawana vipindi kile cha kwanza ilikuwa ni mali ya Ihefu na kipindi cha pili Simba.
Dakika ya 41 Duke Abuya alipachika bao la kuongoza kwa Ihefu akitumia makosa ya safu ya ulinzi lilidumu mpaka dakika ya 70.
Clatous Chama alipachika bao la kusawazisha kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya Kibu Dennis kuchezewa faulo ndani ya 18.
Simba imegawana pointi mojamoja na Ihefu mchezo wao ujao kwenye ligi ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 20 2024.
Ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Simba ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.