Simba

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya kufanyika kwa pambano la Dabi ya Kariakoo, leo kikosi cha Simba kimeanza safari kwenda Zanzibar huku kikizomewa na mashabiki wa Yanga.

Baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam, mashabiki hao na watu wengine waliokuwepo eneo hilo, walianza kuwazomea wachezaji wakati wanaingia eneo hilo.

Simba imeondoka na wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza, akiwemo kipa chaguo la kwanza kwa sasa, Ayoub Lakred aliyekosekana katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu uliopigwa Singida.

Watani hao wa jadi watakutana Jumamosi ikiwa ni mechi muhimu ambayo ina nafasi kubwa kwa timu hizo katika vita ya kuwania ubingwa wa ligi.

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 55 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 46.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here