Moja ya njia bora ya kutaka mafanikio ni kukubali kukuwa, kukubali kubadilika na kuongeza juhudi na wakati mwingine kukubali kuiga mazuri yaliyofanywa na wengine waliyojuu yako kimafanikio na maendeleo pia.
Aliwahi kusema Raisi wa zamani wa Marekani John Kennedy kuwa “Things do not happen, things are made to happen” alimaanisha kuwa “Vitu havitokei, vitu vinafanywa vitokee.”
Hapo sasa ndipo mahali ambapo tupo kwa sasa, vitu ambavyo vilikuwa havifanyiki au hatufanyi kwa sasa vinafanyika, na moja ya sifa ya kutaka kufanya kitu ni kuanza kukifanya kitakupa nafasi ya kujua ni wapi bora nipaendeleze na wapi hapajakaa sawa ni pa boreshe zaidi.
Imetuchukua miaka mingi sana na zaidi ni tokea pale ambapo soka lilianza kubadilika na kuwa inatoa nafasi na pongezi kwa waliyofanya vizuri ndani ya uwanja na nje ya uwanja pia, tumeona viongozi kadhaa wakitunukiwa Tuzo kutokana na uongozi wake alikadhalika tunaona kila kukicha wachezaji nao wakitunukiwa tuzo.
Hapa nyumbani Tanzania soka imekuwa mchezo pendwa sana na kiasi kikubwa ni kutokana na mapenzi makubwa ya mashabiki wengi kwa vilabu viwili vikubwa nchini Simba SC na Yanga SC, kuna nyakati Simba SC walikuwa na Tuzo zao za msimu wanazitoa kwa wachezaji wao waliyofanya vizuri kwa msimu husika kwenye kila nafasi kiwanjani jamboa ambalo kwa kiasi kikubwa iliongeza hamasa, upendo na kujituma kwa wachezaji.
Ni takribani misimu mitano sasa Ligi yetu imepiga hatua kubwa sana hamasa viwanjani imeongezeka, ubora wa wachezaji wazuri na wenye uwezo unaongezeka kila kukicha, udhamini kwa vilabu na matatizo mbalimbali yaliyokuwa yanavikumba vilabu yamepungua kama siyo kuisha kabisa.
Jambo kubwa na la pongezi kwa msimu huu mpya wa 2024/2025 ni maboresho ya haraka au ongezeko la haraka lililotokea kwenye michezo kadhaa ya Ligi iliyochezwa mpaka sasa na jambo ilo siyo lingine bali ni uwepo wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mchezo au mechi ya Ligi kuu, kitu ambacho tulikuwa tunakiona tu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar kwa hapa nyumbani na nje ya mipaka ni kwenye Ligi kuu ya nchini Misri na ligi nyingine kubwa duniani.
Pongezi kubwa sana kwenye eneo ilo iwafikie Bodi ya Ligi kuu Tanzania pamoja na mdhamini mkuu wa tuzo hiyo Benki ya NBC, ni jambo kubwa sana kama taifa kwani siyo jambo dogo ukilitazama kwa ukubwa wake kwani itaongeza ushindani kiwanjani.
Lakini jambo kubwa la kuomba ni muendelezo wa jambo ilo liwe endelevu na la daima kwenye Ligi msimu huu na kuendelea, na hapo ndipo ninapokumbuka msemo wa aliyekuwa raisi wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela alipowahi kusema kuwa “It’s always seems impossible, until it’s done.”