KITAIFA

TUZO YA SIMBA YATOLEWA UFAFANUZI

BAADA ya Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids kuchaguliwa kuwa kocha bora ndani ya Agosti 2024 na Jean Ahoua kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Agosti, uongozi wa Simba umetoa ufafanuzi kuwa kwa namna yoyote ile ilikuwa ni lazima watwae tuzo hiyo kutokana na rekodi zilizoandikwa.

Ipo wazi kuwa baada ya mechi mbili msimu wa 2024/25 Simba imekusanya pointi 6 ndani ya dakika 180 safu ya ushambuliaji ikifunga mabao saba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Mnaonalalamika tuzo ya mwezi zimetolewaje wakati wengine wana mechi moja wengine wana mechi mbili tufanye wote tumecheza mechi moja bado kocha Fadlu ana takwimu nzuri za mechi ya kwanza kuliko kocha yeyote maana alishinda 3-0.

“Jean Charles Ahoua katika mechi ya kwanza alikua na takwimu nzuri kwa kutoa assist kaliiii. Tuache hiyo tutumie mchezo wa mzunguko wa pili bado kocha Fadlu ana takwimu nzuri kwa kushinda mabao 4-0 Ahoua anatakwimu bora katika mchezo huo kwa kuhusika kwenye mabao 3. Mkisema mechi moja moja tunastahili tuzo mkisema mechi zote mbili bado tunastahili tuzo.”

Mchezo wa kwanza ilikuwa Simba 3-0 Tabora United na mchezo wa pili ilikuwa Simba 4-0 Fountain Gate mechi zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button