tetesi za soka ulaya

Liverpool wameungana na Manchester United na Chelsea katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 120m (£102.6m). (O Jogo, via Sport Witness)

Manchester United na Manchester City wanavutiwa na beki wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong, 23. (Sun)

Manchester City wanatazamia kufufua upya azma yao ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham wa Brazil Lucas Paqueta mwenye umri wa miaka 26 msimu huu. (Football Insider)

Leeds United wanapania kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kwa takriban pauni milioni 30 kutoka Manchester City msimu huu ikiwa the Whites watapata nafasi ya kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Sun)

Newcastle itaongeza juhudi ya kumsajili mchezaji wa safu ya ulinzi msimu huu wa joto na kumpa mlinzi Mwingereza Paul Dummett, 32, mkataba mpya baada ya nahodha Jamaal Lascelles kuondolewa kwa hadi miezi tisa kutokana na jeraha la goti. (Newcastle Chronicle)

Kocha wa zamani wa Sheffield United, Paul Heckingbottom anaongoza orodha ya wagombea wanaotarajiwa kuwa meneja wao wa kudumu wa Sunderland. (Sun)

Barcelona wako tayari kupokea ofa ya kumuuza Raphinha msimu huu wa joto ili kupunguza wasiwasi wa kifedha, lakini mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 hataki kuondoka. (Sport – kwa Kihispania)

Tottenham wanapanga kumtoa kwa mkopo Alejo Veliz, 20, kwa klabu tofauti msimu ujao kwani wanahisi mshambuliaji huyo wa Argentina wa Chini ya miaka 20 hajacheza mechi za kutosha katika kipindi chake cha sasa akiwa na Sevilla. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim angependelea kujiunga na Liverpool iwapo atapewa kazi hiyo, lakini atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake mwishoni mwa msimu huu. (Correio da Manha – kwa Kireno)

Tottenham wamejiunga na mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Leeds United, 18, Archie Gray, huku Liverpool pia ikimnyatia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 21. (Football Insider)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here