KIMATAIFA

TETESI ZA SOKA ULAYA – JUMATATU 22.4.2024

Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 27 raia wa Colombia Luis Diaz msimu huu wa joto. (Sport – kwa Kihispania)

Wolves inawazingatia kipa wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 25, mlinda lango wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher, 23, na kipa wa Sunderland Anthony Patterson kamawanaoweza kuziba nafasi ya kipa wa Ureno Jose Sa, 31, anayeondoka kutoka klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun)

Manchester City wako tayari kusikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish mwenye umri wa miaka 28 msimu huu wa joto. (Football Insider)

Barcelona itasikiliza ofa kwa mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 25, msimu huu, huku Manchester United ikionyesha nia. (Sport – kwa Kihispania, kupitia Goal)

Crystal Palace wanaweza kujiunga na harakati za kumsaka kiungo wa kati wa Club Bruges wa Nigeria Raphael Onyedika, 23. (Sun)

Arsenal, Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Real Madrid na Ufaransa Ferland Mendy, 28. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

Borussia Dortmund italazimika kulipakiasi cha kuvunja rekodi ya klabu cha £35m iwapo wanataka kubadilisha mkopo wao kwa mlinzi wa Chelsea Mholanzi Ian Maatsen, 22, kuwa mkataba wa kudumu. (Mirror)

Manchester City wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na Liverpool kumsajili beki wa kushoto wa Wolves wa Algeria Rayan Ait-Nouri. (Mirror)

Vilabu vingi vya Premier League vinafikiria kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid Mhispania Samu Omorodion, 19, ambaye yuko kwa mkopo Alaves. (AS – kwa Kihispania)

Arsenal italazimika kulipa euro 60m (£51m) ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 kutoka Juventus msimu huu wa joto. (Tuttosport – kwa Kiitaliano)

Newcastle wanapanga kumnunua mlinzi wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 wa Juventus Dean Huijsen ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Roma kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Manchester United na Newcastle huenda zikamnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ikiwa hatasaini mkataba mpya na Juventus msimu huu wa joto. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

Leeds huenda ikakubali ofa ya karibu pauni milioni 30 kwa winga wa Italia Wilfried Gnonto, 20, ambaye anavutia vilabu kadha vya Premier League. (Football Insider)

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button