tetesi za soka

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi ndiye mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya Ten Hag ikiwa ataondoka Old Trafford, na Seagulls wanamfikiria kocha mkuu wa Burnley Vincent Kompany kama mbadala wake. (Teamtalk)

West Ham watafanya mazungumzo na kocha mkuu wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, 39, huku wakiamua iwapo wataongeza mkataba wa David Moyes msimu huu wa joto. Haijabainika ni wapi Wana Nyundo wangeshika nafasi katika chaguzi za Amorim. (The Athletic)

Kocha wa zamani wa Wolves Julen Lopetegui ni mshindani mkubwa kuchukua nafasi ya Moyes kwenye Uwanja wa London Stadium. (Telegraph)

Amorim anasalia kuwa chaguo la kwanza la Liverpool kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp lakini meneja wa Brentford Thomas Frank anazingatiwa ikiwa Mreno huyo ataenda kwingine. (Team Talk)

Uwezo wa Erik ten Hag utatathminiwa na mkurugenzi mpya wa kiufundi wa Manchester United Jason Wilcox kabla ya klabu hiyo kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa Mholanzi huyo. (Telegraph)

Klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr bado ina nia ya kumsajili Kevin de Bruyne wa Manchester City msimu wa joto na inatarajiwa kuwasiliana na kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 32 hivi karibuni. (Rudy Galetti)

Barcelona wamejiunga na Arsenal kutaka kumnunua mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 24, mwenye thamani ya pauni milioni 90, huku klabu hiyo ya Uhispania ikitarajia kufanya makubaliano huku Magpies wakitafuta kufuata sheria za usawa wa kifedha. (Sun)

Arsenal na Manchester United wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa Crystal Palace na Ufaransa Michael Olise, 22, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea, Manchester City na Juventus . (Football Insider)

Arsenal wanatarajia kuongeza wachezaji watatu au wanne msimu huu wa joto huku wakikamilisha kufanyia marekebisho kikosi chao,naye mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 25, akiwa lengo lao kuu. (Footbal Transfer)

Liverpool walimtazama Gyokeres katika ushindi wa 3-0 wa Sporting dhidi ya Vitoria wikendi huku wakilenga mshambuliaji mpya na beki wa kati msimu huu wa joto. (HITC)

Manchester United imemfanya beki wa Everton na England mwenye umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, kuwa lengo lao kuu msimu huu na wanataka kukubaliana mkataba wa mapema. (Football Insider)

Real Betis wanalenga kumsajili mlinda lango wa zamani wa Manchester United na Uhispania David de Gea, 33, ambaye amekuwa mchezaji huru tangu kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu uliopita. (Estadio Deportivo – kwa Kihispania)

Beki wa Brazil Thiago Silva, 39, ataondoka Chelsea mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Fabrizio Romano)

Crystal Palace wanavutiwa na kiungo wa kati wa Leicester City na Nigeria Wilfred Ndidi, 27, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (sport)

Bayern Munich wanafuatilia hali ya mchezaji wa Barcelona Frenkie de Jong, ingawa mshahara wa kiungo huyo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 unaweza kukatiza uhamisho wake. (Sky Sports Ujerumani)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here