Kocha mkuu wa klabu ya Coastal Union, David Ouma ameipa heshima klabu ya Yanga kuelekea mchezo wao wa leo wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Ouma ameeleza kuwa klabu hiyo ilikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika kulingana na aina ya kikosi walicho nacho lakini hiyo haiwazuii wao kufanya vizuri.
“Yanga ni timu iliyokuwa na uwezo wa kubeba Ligi ya mabingwa Afrika, ni timu iliyokamilika.”
“Kesho sisi Coastal Union tutatengeneza nafasi zaidi ya Tano, wachezaji wangu wanao huo ubora, tunajua sehemu ambayo tutautawala mchezo.”
–David Ouma, Kocha mkuu wa Coastal Union kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Yanga.