KITAIFA

SAMATTA NA MSUVA WATEMWA STAIFA STARS, JOB AREJESHWA

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea.

Kikosi hicho kitaingia kambini bila ya mastaa Mbwana Samatta na Simon Msuva ambao hawajaitwa.

Samatta na Msuva wametemwa kikosini huku beki Dikson Job akirudishwa baada ya kuwapo na tetesi za kuwa na sintofahamu na kocha huyo.

Morocco alitolea ufafanuzi ishu ya Job akisema, “Mimi na Job tumezungumza yameisha salama.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button