UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba umejifunza jambo la muhimu sana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union licha ya kupata ushindi wa bao 1-0.


Aprili 27 2024 Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union baada ya dakika 90 walikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao la Joseph Guede.


Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 62 baad ya kucheza mechi 23 msimu wa 2023/24.


Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari Yanga ameweka wazi kuwa wachezaji walifanya kazi kubwa kusaka ushindi jambo ambalo limewezekana.


“Ilikuwa kazi kubwa dhidi ya Coastal Union na mwisho tumepata pointi tatu muhimu, tunazidi kufanyia kazi makosa na Coastal Union wametupa somo kuhusu mechi za mwisho ambazo zina ushindani mkubwa.


“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa ajili ya mechi ambazo zimebaki malengo yetu ni kuona kwamba tunafanikiwa kutwaa taji la ligi,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here