MWAMBA Khalid Aucho kiungo wa Yanga amewataka wapenda soka kumfurahia wakati huu akiendelea kulisakata kabumbu katika ligi ya Tanzania kwasababu hakuna Khalid Aucho mwingine ambaye ataonekana kwenye soka la Bongo.


Nyota huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabilia Tabora United kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali Uwanja wa Azam Complex.


Kupitia kwenye ukurasa wake wa Insta ameandika namna hii: “Nifurahie wakati huu nikiwa kwenye ligi ya Tanzania, kwasababu hautomuona Aucho Khalidi mwingine tena. Muwe na wiki mpya yenye baraka,”.


Huu ni msimu wa tatu kwa Aucho tangu ajiunge na Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 kibindoni baada ya kucheza mechi 24.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here